Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleSiasaTundu Antipas Mughwai Lissu

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Tundu Antipas Mughwai Lissu

Mwanasiasa na Makamu Mwenyekiti CHADEMA

Ss
Tarehe ya Kuzaliwa:
1968-01-20
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Tundu Antiphas Mughwai Lissu, amezaliwa tarehe 20, januari mwaka 1968 katika wilaya ya Ikungu iliyopo mkoa wa Singida. Kitaaluma ni Mwansheria, tena wengi hupenda kumuita Mwansheria Nguli.

Ni mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanzania TLS.

Amesoma katika shule ya Iliboru iliopo Mkoa wa Arusha na kuhitimu mwaka 1983.

KAZI

Alianza kufanya kazi kama Mwansheria katika ofisi za Enviromental Action Team LEAT, kisha akahamia ofisi ya Word Resource Institute kama Wakili, amefanya kazi nyingi za Uwakili katika masuala ya utetezi wa Hakiza binadamu.

SIASA

Alianza siasa mwaka 2010, alipo chaguliwa kuwa Mbunge wa Singida Mashariki. Katika safari ya siasa zake, Lissu amejijenga katika siasa za kutobadilika, misimamo yake ni ile ile, anasifika kwa kuwa kiongozi mwenye upinzani wa kweli.

Mara kadha amewahi kufanya utafiti na kuibua mapungufu katika manunuzi mbali mbali ya kiserikali, uhujumu uchumi na ufisadi, aliziita tafiti hizo "LIst of Shame".

Tundu Lissu, alikamatwa zaidi ya mara 5 mwaka 2017 pekee, akituhumiwa kwa makosa ya kumtukana Hayati Magufuli, na kuvunja sheria kwa kufanya mikutano ya wazi ya siasa iliyopigwa marufuku nchi nzima.

Tarehe 23 Agosti 2017 Jeshi la Polisi lilifanya msako mkali nyumbani kwake, kisha alikamatwa kwa kosa la kumuita Hyaai Magufuli "Dikteta Uchwara"

Alikamatwa kwa kufuatia kutangaza kwa umma kuwa ndege zilizonunuliwa kutoka nchini Canada hazikunuliwa kwa Fedha Taslimu kama ilivyotangazwa bali zilikuwa kwa mkopo.

SHAMBULIO

Majira ya mchana wakati wa maoumziko ya kikao cha Bunge, tarehe 7 mwezi septemba mwaka 2017, alishambuliwa akiwa ndani ya gari lake nje kabisa ya nyumba za Wabunge, eneo ambalo linaaminika kuwa na usalama mkubwa.

Alijeruhiwa vibaya sana na watu ambao hadi hii leo hawajafahamika n, lakini wiki chache kala ya shambulio hilo, Lissu alitangaza wazi kuwa kuna watu wanamfatilia .

Alipewa huduma ya kwanza katika hospitali ya Mkoa ya Dodoma, kisha alisafirishwa haraka hadi hospitali ya Agha Khan iliyopo jijini Nairobi nchini Kenya.

Alipatiwa matibabu kwa miezi kadhaa katika hospitali hiyo kabla ya kuhamishiwa nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu ya kina.

Akiwa Ubelgiji alifikishwa katika hosipitali ya Chuo kikuu cha Leuven kilichopo Gasthuisberg, inaelezwa kuwa akiwa huko alifanyiwa opresheni 19 za kuokoa maisha yake.

Chama chake kilitoa taarifa ya wazi na kutuma ujumbe kwa Hayati Magufuli kuhusu shambulizi hilo huku wakisema bayana kuwa lilikuwa ni shambulizi la kisasi cha siasa.

Hayati Magufuli alituma salamu za pole na alistushwa na tukio hilo huku akiviagiza vyombo vya dola kufatilia kuhusu undani wa shambulizi hilo.

Tarehe 27, julai mwaka 2020, Lissu alirejea Tanzania, moja kwa moja kuja kugombea nafasi ya Urais.

Baada ya uchaguzi kuisha alirejea nchini Ubelgiji .

TanzaniaWeb