Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleMkuu wa NchiYoweri Museveni

Watu Maarufu Tanzania

Mkuu wa Nchi

Yoweri Museveni

Rais wa Uganda

MUSEVENI1
Tarehe ya Kuzaliwa:
1944-09-15
Mahali pa Kuzaliwa:
Uganda

Yoweri Kaguta Museveni, amezaliwa septemba 15 mwaka 1944 katika ardhi ya uganda, amewahi kuwa Afisa mwandamizi wa Jeshi kabla ya kuchaguliwa kuwa rais wa nchini humo kuanzia mwaka 1986. ELIMU

Safari yake ya elimu ilianzia katika shule ya msingi Kyamate kisha akajiunga shule ya sekondari ya Mbarara alipofanikiwa kuendelea na elimu ya juu kwa maana ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondary Ntare.

Amesoma katika chuo kikuu Dar es Salaam kilichopo Tanzania, japo hakuna taarifa zinazothibitisha kuwa amewahi kusoma hapo. hata hivyo anaeleza kuwa alisoma masomo ya uchumi, pamoja sayansi ya siasa.

Akiwa chuoni alijihusisha na harakati zakisiasa kwa wakati ule zilijulikana kama Pan-African Politics, aliweza kuanzisha harakati za mapinduzi ya wazi akiwahusisha wananfunzi wenzie wakati wakiwa chuo, harakati alizoziita "Univeristy Students' Revolutionary Front activist Group.

KAZI

Mwaka 1966-1980 alikuwa mstari wa mbele katika kufanya maoinduzi ya kumuondoa rais aliyekuwa madarakani kwa wakati ule, Idd Amin Dada, Mapinduzi hayo yalifanyika mwaka 1972 chini ya usaidizi wa jeshi ka Tanzania. na hapo baadae aliunda chsma chake cha Front for National Salvation mwaka 1973. Katika kipindi chote cha mapambano dhidi ya Iddi Amin, Museveni alikuwa mstari wa mbele katika kupambana na kuna wakati ilimlazimu kuyakimbia makazi yake, kwa sababu ya vitisho kuzidi. Alishiriki Mapinduzi haya kwa kushirikiana na Hayati Mwalimu Nyerere, hadi walipofanikiwa kumuondosha kabisa kiongozi huo mwaka 1979, ndipo Museveni aliporejea tena nchini mwake kuendeleza mapambano. Kwanini kuendeleza mapambano kwa sababu, baada ya kumuondoa Iddi Amin, uliingia utawala wa Milliton Obote mwaka 1980, huu haukuwa utawala mzuri, Museveni kwa kushirikiana na wapambe na wafuasi wake walianzisha harakati za kuondosha utawala ule. Walianzisha kikundi walichokiita National Resistance Army, ili kuweza kupambana na utawala huu, na hakika walifanikiwa kwa kiasi kikubwa, kwani huu utawala haukuweza kudumu kwa muda murefu.

SAFARI YA URAIS

Mwaka 1986 alichaguliwa kuongoza taifa hilo, chini ya chama chake cha Nationa Resistance Army (NRA), matumaini ya Waganda yarirejea rasmi .

Historia inaweka wazi hili, kuwa Museveni alipata wafuasi wengi karibia nchi nzima, hii ni kutokana na mwenendo wa siasa alizokuwa akizifanya kwa wakati ule. Aliwaahidi wananchi nwake amani, kuboresha ulinzi katika mipaka yote, na uhuru kurejea tena nchini humo. AWAMU ZA UONGOZI

Mwaka 1996-2001 (ushindi wa asilimia 75) Katika awamu hii Museveni alifanikisha, elimu ya msingi kuwa bure, aliboresha sekta ya afya ya nchini humo iliyokuwa imezorota kufuatia kukithiri kwa utawala wa kidikteta.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2001 katika uchaguzi mkuu, Museveni alipata upinzani mkali kutoka kwa mpinznai wake Bisgeye. lakini aliweza kutetea kiti chake kwa ushindi wa aslimia 69.

Nikurudishe nyuma kidogo, kati ya mwaka 1996 , aliweza kutambulika kimataifa zaid, pale alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika(OAU), katika kipindi hiki aliweza kuongoza kikamilifu kampeni ya mapambano dhidi ya Ukimwi barani Afrika.

Mwaka 2001-2006 Alishinda nafasi ya Urais kwa mara nyingine tena aliwalaza hoi wapinznai wake katika chati za matokeo ya urais nchini humo. Lakini ushiriki wake katika nafasi hii kwa awamu hii ulikuwa kinyume na Katiba ya nchi hiyo, kwani alikuwa hana sifa za kuendelea kuliongoza taifa hilo kwa mujibu wa katiba. Museveni alianza kampeni za chinichini za kubadili kipngele cha ukomo wa miongo miwili ya utawala, ili aweze kuendelea kuwa Rais.

Umoja wa mataifa na nchi wanachama wa umoja wa Afrika waliingilia kati suala lakini hakuna kilichozaa matunda.

Mwaka 2006-2011 Chama cha NRA kilimteua tena Museveni kugombea kiti cha urais, katika kipindi hiki mpinzani wake mkuu Bisigeye alikamatwa na kuwekwa ndani kwa tuhuma za ubakaji na uhujumu uchumi, lakini aliweza kuachiwa huru baada ya ushahidi kukosekana. Museveni alishinda tena kwa asilimia 59 dhidi ya mpinzani wake Bisegeye aliyekuwa na assilimia 37.

Mwaka 2011-2016 Alishinda kwa asilimia 68, licha ya kuwa wapiga kura waliosajiliwa walikuwa asilimia 59 tu, jambo hili liliwashtusha watu wengi, wasimamizi wa kimataifa walicharuka huku wakiiushutumu uchaguzi kuwa wa ubadhilifu.

Katika awamu hii, kulitokea mfumuko mkubwa bei za bidhaa, mafuta, chakula vikawa havishikiki nchini humo. Uhuru wa habari nao ukaanza kuyoyoma, matukio ya mauji na vitisho wa waandishi wa habari yalizidi, shirika la Haki la binadamu, liliripoti matukio 50 ya kikatili yaliyofanywa na serikali dhidi ya waandishi wa habari.

Mwaka 2016-2021 Katika awamu hii, Rais Museveni, amepitisha miswada mbali mbali ya sheria ambayo mpaka sasa inapigiwa kelele kwa ukandamizaji mkubwa.

Muswada wa mwaka 2008, UKOMO WA UMRI WA KUGOMBEA URAIS Muswada ulipitishwa tarehe 27 disemba 2017, katika muswada huu, kigezo cha umri wa kugombea uraais kilitupiliwa mbali. apo awali ilikuwa ni kuanzia miaka 35 hadi 75, pia umeongeza muda wa bunge na urais kutoka miaka mitano hadi saba.

Mwaka 2021 Uchaguzi wa mwka 2021, ulikuwa wa tofauti, hapa Rais Museveni alipokea upinzani mkli kutoka kwa Mgombea kijana na Mwanamuziki, Bob wine, lakini alifanikiwa kushinda kwa asilimia 58.6

TanzaniaWeb